MBOKA NA BISO
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 794
- 793
Kenya imepiga hatua muhimu katika sekta ya afya, baada ya kupewa leseni ya kushiriki uzalishaji wa dawa mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV inayojulikana kama Alimatravir, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa dawa hiyo kwa gharama nafuu katika nchi nyingi za Afrika.
Kampuni ya dawa ya Merck imetoa leseni kwa kampuni saba duniani kutengeneza toleo la bei nafuu la dawa hiyo ya kila mwezi ya kuzuia HIV, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Universal Corporation Limited (UCL) ya Kenya. Hata hivyo, uzalishaji huo utaanza rasmi endapo majaribio ya kitabibu yanayoendelea yataonyesha kuwa dawa hiyo ni salama na yenye ufanisi.
Kwa sasa, majaribio ya hatua ya mwisho yanaendelea nchini Kenya, Uganda na Afrika Kusini, yakiwahusisha wasichana na wanawake vijana kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali za afya.
Akizungumza katika mkutano wa kando wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Kenya William Ruto amesema ushiriki wa Afrika katika utengenezaji wa dawa mpya ni hatua kubwa kuelekea kujitegemea katika sekta ya afya na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya bara hilo.
Iwapo itaidhinishwa rasmi, alimatravir inaweza kuwa dawa ya kwanza ya kila mwezi ya kumeza kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya HIV.
Maswali:
1. Unadhani Afrika itanufaikaje ikiwa itaongeza uwezo wake wa kutengeneza dawa badala ya kutegemea uagizaji kutoka nje?
2. Je, hatua hii inaweza kusaidia kupunguza maambukizi mapya ya HIV barani Afrika?