Hii ndo nchi pekee duniani isiyotawalika

Hii ndo nchi pekee duniani isiyotawalika

Chegge

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
194
Reaction score
7
Vuta picha unaamka asubuhi katika jiji ambalo sheria pekee inayotembea barabarani ni mlio wa risasi. Hakuna polisi wa kumpigia simu ukivamiwa.

Hakuna mahakama ya kukimbilia ukidhulumiwa. Kila kona ya mtaa ina "mbabe" wake, kila kizuizi barabarani kina kodi yake, na usalama wako unategemea tu ukoo uliotoka au nguvu ya mtutu ulioshika mkononi.
Hii siyo movie Hii hali halisi Somalia, nchi ambayo kwa zaidi ya miongo mitatu, dunia imeitazama na kujiuliza swali moja gumu: Kwa nini nchi hii haitawaliki?

Kila kitu kilianza kuporomoka mwaka 1991.
Siku ambayo utawala wa dikteta Siad Barre ulipoanguka, hakukuwa na mtu wa kushika usukani. Taasisi zote za serikali zilifutika usiku mmoja kama moshi. Wanajeshi waligeuka wababe wa kivita kila mtu na kundi lake, silaha za Vita Baridi zilizomiminwa na mataifa makubwa zikaingia mikononi mwa raia, na nchi ikapasuka vipande vipande.

Lakini hapa ndipo panapotisha zaidi...
Wakati dunia ikidhani amani ingerudi, giza nene zaidi liliingia.
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab liliibuka kutoka kwenye majivu ya vita na kujenga "serikali kivuli" katikati ya msitu na vijiji.
Leo hii, wakati serikali kuu ya Mogadishu ikilindwa na majeshi ya kigeni kwenye ngome zake, Al-Shabaab wanatoza kodi mpaka kwa wafanyabiashara wakubwa, wanaendesha mahakama zao za gizani, na yeyote anayethubutu kukaidi amri zao... anapotea bila alama, huko sheria ni msumeno.

Na kana kwamba hiyo haitoshi, hata ndani ya mfumo wa siasa, kila koo inavutia kwake. Mfumo wa kugawana madaraka kwa koo (maarufu kama 4.5 Formula) umefanya wanasiasa wengi wajali matumbo ya koo zao badala ya taifa. Serikali kuu na majimbo yake hayana kauli moja, kila koo inajitawala kivyake, na serikali haina la kufanya, koo hasimu kila siku zinakiwasha.
Mambo yalipokuwa magumu, sehemu moja iliamua kujichukulia sheria mkononi na kuanza kujitawala yenyewe ndani ya Somalia na kujiita Somaliland huko ndio kuna amani na kunakalika. Walifanya hivyo mwaka 1991.
Kiufupi Somalia inakaa namna hii, Serikali inapigana na Al shaabab na Koo baadhi, Al shaabab inapigana na serikali na koo baadhi, Koo nazo zinapigana zenyewe kwa zenyewe na serikali na Al shaabab pia. Huku bado kuna Maharamia nao wana siraha, serikali ikibanwa inapigana nao tena.
Ukiitazama Somalia leo, unagundua ukweli mmoja mchungu:
Nchi haifi kwa kukosa rasilimali, Somalia ina pwani ndefu zaidi barani Afrika, ina madini, na ina watu wanaozungumza lugha moja na dini moja. Nchi hufa pale dola inapokufa, na hofu inapochukua nafasi ya sheria.
 
Back
Top Bottom