Njia za kuepuka ndugu wasihamie kwako moja kwa moja hizi hapa.

Njia za kuepuka ndugu wasihamie kwako moja kwa moja hizi hapa.

MBOKA NA BISO

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
794
Reaction score
793
1. Hakikisha wageni ambao ni mke na mme hawalali chumba kimoja. ( Mimi kwangu dada yangu au mtu yeyote anayekuja kwangu na mkewe huwa nawapangia vyumba tofauti vya kulala, mwanaume analala chumba cha nje na mwanamke alale na house girl) kutokana na kero hii huwa hawachelewi kuaga.

2. Mgeni bachelor wa kiume hakikisha analala chumba cha ndani kabisa ili asipate muda wa kujinafasi kwenda kuangalia mipira (usithubutu kumpa chumba cha nje itakuwa furaha sana kwake atajisahau)

3.Kama huna vyumba vya kutosha wapeleke wakalale gest ( waulize wanakaa siku ngapi halafu lipia)

4. Usiwatambulishe wageni kwa mbwa wako, ( wabaki na hofu ya mbwa hadi watakapoondoka)

5. Mama mwenye nyumba usimpe zamu mgeni wa kike apike (asije akalizoea jiko akasahau kurudi kwao wacha asijisikie huru)

6. Kuku usichinje waambie wamepewa chanjo...au wanataga
 
Yote hayo unajitesa bure! Usikubali wakuzoee , unaenda kumtembela ndugu huna Cha kufanya huko kwenu?
Wenye shida msaidie huko aliko! Lakini pia epuka kuoa familia/ kabila za watu wavivu na wanaoona umasikini ni jambo la kawaida!
 
Back
Top Bottom