Marekani yatoa muongozo wa makubaliano kati ya Rwanda na DRC

Marekani yatoa muongozo wa makubaliano kati ya Rwanda na DRC

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,494
Reaction score
1,466
Massad Boulos, mshauri mkuu wa serikali ya Marekani, kuhusu maswala ya Africa, ametangaza kuwa baada ya Rwanda na DRC kuwakilisha matakwa ya kila upande kuhakikisha nchi hizi mbili zinafikia makubaliano ya amani,
Marekani imeandaa na kukabidhi muongozo wa amani baina ya nchi hizi mbili,kwa mawaziri wanaohusika; kwa ajili ya kuyapitia na kutoa mrejesho kama watakubaliana nayo au wataomba yafanyiwe marekebisho.

Sawali la kujiuliza: Kama nchi zenyewe hazina uwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili, nchi hizi, jumuia zinazowakutanisha kama EAC, zikawa hazina uwezo, nchi jirani ndo ikawa hamna kitu, Umoja wa Afrika ukawa hauna msaada, mpaka nchi furani,kiubabe tu imeamua kudraft makubaliano na yanatakiwa yasainiwe, uhuru tunaouimba Africa upo wapi?

Si hapa kama mtindo ndio huu,maendeleo tuyaone tu kwenye runinga na magazetini, wababe wanufaike? Mnaozaa, vizazi vijavyo vitaishi wapi, kwa misingi ipi, na maisha gani?

Hii ni aibu!!!!


Pia ikumbukwe, Marekani aliziomba nchi hizi mbili kwanza kuwa tayari kusaini makubaliano ya uwekezaji, ambayo pia Marekani imesema yameshaandaliwa, na wakati wowote yatakapidhiwa serikali hizo ili yapitiwe, na yatiwe saini ya mwisho mnamo June mwaka huu, huko Ikulu ya Marekani, mbele ya rais Donald trump.

La kuongezea, habari zinazoendelea mpaka sasa, ni kwamba baada ya MONUSCO kutoka nchini DRC,maeneo ambayo itakuwa inaangalizia usalama, yatakuwa chini ya uangalizi wa kundi la mamruki,kutoka Marekani, lijulikanalo kama BLACKWATER.
 
Back
Top Bottom