Tabia ya nyoka black mamba anapokutana na binadamu

Tabia ya nyoka black mamba anapokutana na binadamu

Chegge

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
194
Reaction score
7
Mtaalamu wa wanyama anayejulikana kama Pete Kessy amesema;

"Watu hawapaswi kuogopa wanapomuona Black Mamba au Koboko kwa sababu hanga'ati moja kwa moja kama tunavyofikiria.

Kwanza, mnapokutana ana kwa ana, hakukimbizii kama tunavyodhani. Badala yake, huanza kutafuta shimo lake ili akimbilie kujificha. Anapoanza kukimbia, watu wengi hudhani anakukimbiza, kumbe anakimbilia kwenye shimo lake.

Wakati mwingine unaweza kuwa umesimama karibu na shimo lake, hivyo atalazimika kuinua kichwa na kufungua mdomo kuashiria hatari. Hiyo ni tahadhari tu, wala si kwamba analenga kukudhuru.

Hata hivyo, katika harakati za kutafuta shimo lake, anaweza kukuuma na sumu yake ni hatari kwa sababu hushambulia mfumo wa fahamu.

Hivyo, ukitulia unapomuona, atahangaika kutafuta njia ya kujificha na hatimaye kuingia kwenye shimo lake.

Hayo mengine unayosikia huwa ni uongo."
 
Back
Top Bottom