Kwa lugha rahisi, wa kwanza anaetakiwa kufa humo ndani, ni wewe brother..

Kwa lugha rahisi, wa kwanza anaetakiwa kufa humo ndani, ni wewe brother..

Cyurinyana

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
45
Reaction score
36
Nyoka akiingia ndani ya nyumba, mkeo na watoto watakimbilia mgongoni kwako..

Kimsingi wanaamini wewe ndio una uwezo wa kupambana nae..

Lakini kikanuni, hata wewe una hofu, na unajua kuwa huyo mdudu humuwezi..

Kwa lugha rahisi, wa kwanza anaetakiwa kufa humo ndani, ni wewe brother..

Ukikimbia tu, wale uliowaacha wanaamini nyoka hana madhara, kuliko mbio za Baba..

Ni umuue nyoka ili mkeo akakusifie saluni, na watoto wakatambe shuleni..

Lakini kwa lugha ya ulimwengu, wewe ndio shujaa bora wa hiyo nyumba..

Haujawa mwanaume kwa bahati mbaya, ni mchakato uliotumia muda mwingi sana..

Kuna muda wewe ni mlinzi, kuna wakati wewe ndio mwizi mwenyewe, inategemea unaishije na unaowaongoza..

Unaweza kuwa mume, na ukijipindua kidogo ukawa mpuuzi mmoja, anaeongeza idadi ya watu humo ndani..

Iwe ni kwa changamoto, dharau, kutoonekana umuhimu wako, au kupuuzwa, daima usisahau, wewe ni mwanaume..

Dunia imeumbwa kukuzunguka wewe, na wewe usiizunguke Dunia, ukaenda kinyume chake..

Haijalishi unapitia nini, ila ukipata nafasi ya kuwa mwanaume, usiichezee..
 
Back
Top Bottom