Kongole kwa ndugu wanaotambua jitihada za ndugu waliowapambania

Kongole kwa ndugu wanaotambua jitihada za ndugu waliowapambania

Chegge

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
196
Reaction score
7
Mimi ni kijana wa 26yrs tumezaliwa 6 kwenye tumbo la mama.
Wakati nakua mzee alikuwa na wake 4 kwa bahati mbaya mama yetu alifariki kipindi bado watoto hivi, tukalelewa na mama zetu wa kambo kila mmoja alienda aliko ona panamfaa,basi bwana.

Sasa katika harakati za kusoma nilipofika F3 mzee akanipeleka shule ya private nikahitmu F4 sikurudi home, nikaingia mtaani .
Matokeo yalipo toka nimepasua ikanibidi niunge advanced sikurudi home mpaka namaliza F6 likizo zangu zilikuwa ni pale pale shule, baada ya kumaliza 6 nikaunga jkt sikurudi home japp mzee tulikuwa tunakutana tuu akinivuta kweny mishe zake.
Baada ya kumaliza jkt matokeo yakawa yametoka namshukru MUNGU nilipasua harakati za kwenda chuo hazikufanikiwa kipindi hiko niko kwa bro wa upande mwingine.
Basi niliposhindwa kwenda chuo sikuweza kukaa pale kwa bro kutokana na majukumu niliyokuwa nayo na wadogo zangu watatu nao walikuw tayari wako shule ikabidi nitafte kazi.

Kwa mara yangu ya kwanza naenda Dar kikazi nikafikia kwa baba'angu mdogo nilizurula saana town kutafta kazi sikupata; kila nilipofika niliombwa kitambulisho(sikuwa nacho), baadae kuna baba angu mdogo akaniunganisha kazi ya kukata mkaa pwani nikawa nimeenda huko, mwaka wa kwanza nikapiga ile kazi huku hela ninanyo ipata inaenda kusaidia wadogo zangu shule, mimi, na mtoto wangu maana kipind niko kwa bro katika kuruka ruka nikamtia mimba binti wa watu.
Baada ya wadogo zangu kuhitimu shule mwaka wa pili huo nikawa huru sasa nikakutana na mdada nikampenda , kutokana na upweke, stress za kukosa ada na changamoto za maisha nikamvuta aje tuishi, akaja tukaishi kama mke na mme

Mwaka ukakatika sifanikiwi na kazi napiga kama nimetumwa na kijiji kila nilipopata hela ndugu wnakua ni kama kuna mtu kawaambia kuwa nina hela, simu zinakua ni nyingi, cha kushangaza kila nilipopata hela lazima niugue, kwa mwezi nilikuwa na uwezo wa kutengenza mpaka 400k ila mpaka mwezi uishe hiyo hela haipo nina miti tu ya kuchoma mkaa basi bwana, maisha yakasonga.

Sasa mwaka huu mwezi wa 6 nilipishana kidogk na mwenzangu akawa ameenda kwao, hazikupita siku nyingi nikawa nimeugua saaana nikamcheki aje kuniuguza.

Alikuja kukaa siku mbili tu akaaga anaenda kwa dada'ake, nimeugua kwa mda kias kwamba nikawa sina uwezo wa kufanya kazi yeyote ( shida ya moyo) nikatumia hela ya saving yote mpaka ikakaribia kuisha ikabidi nimcheki mzee akanifosi nirudi nyumbani, sasa narudije na hela sina na ukizingatia nina zaidi ya miaka 7 sijawahi kurudi???

Basi mzee ikabidi awape taarifa ndugu zangu wote wa upande wa mama wengine kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kunisaidia ikabidi mdogo wangu wa tumbo moja akauze asset zake kunisaidia kaka'ake nirudi home.

Baada ya kufika home nimekuta madogo niliowaacha wako primary wameoa na wengine wametusua( hapa nawapongeza asee😆🙏)

Kinachonipa changamoto ni kwamba baada tu ya mimi kufika nyumban yule mke wangu kaolewa hata nyumban kwao nimepiga simu hawajui kama binti yao kaolewa inauma mno😭😭 .

Na kuna wadog zangu wawili wa kike niliwaahidi nitapambana nihakikishe wanaenda shule watimize ndoto zao niliwaahid siku wameniona niko nyumban basi wajiandae kwenda chuo kwa bahat mbaya sijawakuta nyumbani walikimbia mateso ya mama wa kambo wako huko wanafanya kazi za kulipwa elfu moja kwa siku dingi hata hawazi.
Mimi kama kaka mkubwa naumia saana watu wanaosubili kushangilia ushindi wangu mpaka sasa half time ubao unasoma 3_0😭😭, niko nyumban sasa miaka mingi sipo nimerudi na nguo zangu tu sina chochote, kila wakati nikiona madogo wanapiga simu kuuliza hali yangu ya kiafya naona kabisa sauti zao hazina furaha ni za maumivu mno mimi ndo jembe lao kwenye kila shamba lao, sitamani waharibikiwe kabisa na dunia hii ya leo waliniahidi watajitunza wakiningojea niwapeleke hata veta leo mimi nimeshindwa kutimiza ahadi yangu kwao.

Nahisi kama dunia imenitenga sina hata mtu ambae naweza kumueleza maumivu ninayo pitia, sina mdau wa kunipa mchongo, washikaji zangu ndo kabisa wanaishia kunipa salamu badala ya michongo, siwezi kuwalaum nao wana changamoto zao yawezekana.

Nimekuja kwenu naomba mwenye kazi yeyote anipe nifanye walau niepuke hii aibu ya kuchekwa na wadogo zangu lakini pia niwaokoe dada zangu niwapeleke hata chuo cha ufundi tuu wasije haribikiwa nikiwa naona, nakosa hata amani nikiwa hapa nyumbani naomba saana kama una kazi yeyote nipe nifanye as long as haina madhara kwa Mungu wangu, kwangu na kwa jamii inayonizunguka🙏🙏
 
Back
Top Bottom