Kisa cha mwanaume alielea watoto 3 kwenye ndoa,akidhani wake,kumbe hana hata 1 kati yao

Kisa cha mwanaume alielea watoto 3 kwenye ndoa,akidhani wake,kumbe hana hata 1 kati yao

Chegge

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
196
Reaction score
7
Richard na mkewe waliishi pamoja kwenye ndoa yenye furaha na amani kwa zaidi ya miaka ishirini huko Uingereza.
Walijaliwa kupata watoto watatu wakubwa, na majirani zao waliwasifu kama familia bora na yenye upendo mkubwa.

Richard alikuwa akifanya kazi kwa bidii kuhakikisha mkewe na wanawe wanakula vizuri na kusoma shule nzuri.

Tatizo lilianza siku moja Richard alipokwenda hospitali kufanya vipimo vya kawaida vya afya kabla ya kusafiri kikazi. Katika vipimo hivyo, daktari alimwambia jambo ambalo hakulitegemea maishani mwake.

Daktari alimueleza kuwa kutokana na tatizo la kimaumbile alilozaliwa nalo, Richard hakuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito tangu alipozaliwa.

Richard alidhani daktari amekosea majibu. Alikwenda hospitali nyingine kubwa zaidi na kupima mara mbili, lakini majibu yalikuwa yaleyale: hakuwahi kuwa na uwezo wa kupata mtoto maishani mwake.

Hapo ndipo akili yake ilipovurugika. Alirudi nyumbani akiwa haamini anachokiona. Aliwatazama watoto wake watatu aliowalea na kuwasomesha kwa jasho lake kwa miaka zaidi ya ishirini, kisha akamtazama mkewe aliyekuwa akimwamini kuliko mtu yeyote duniani.

Alipomuuliza mkewe ukweli mbele ya vipimo vya daktari, mwanamke huyo aliangua kilio na kukiri kuwa watoto wote watatu hawakuwa wa Richard, bali alizaa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa familia yao.

Richard alipata mshtuko mkubwa na kuamua kuvunja ndoa hiyo mara moja. Kesi ilikwenda mahakamani, na mahakama ilimwamuru yule mwanamke kumlipa Richard fidia kubwa ya pesa kwa kumdanganya na kumlea watoto wasio wake kwa miaka yote hiyo.

Hata hivyo, jambo lililowaumiza watu wengi ni kwamba licha ya kugundua ukweli huo mchungu, watoto wale walikataa kumwacha Richard, wakidai kuwa yeye ndiye baba yao wanayemjua tangu utotoni.
 
Back
Top Bottom