MBOKA NA BISO
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 794
- 793
Mwaka 1997, Kijana Mwenye Umri wa Miaka 26 tu aitwaye Joseph Kabila alishika bunduki akishirikiana bega kwa bega na Wanajeshi wa taifa la Rwanda kuingia Kinshasa na kufanikisha kumuweka baba yake Madarakani.
Mwaka mmoja baadaye, 1998, Laurent-Désiré Kabila, aliwafukuza kwa aibu Warwanda hao hao na kuwaita Wavamizi katika nchi ya Congo. Miaka mitatu baadaye, Januari 16, 2001, Laurent Kabila aliuawa Ikulu kwa risasi tatu za kifuani na mlinzi wake wa Karibu sana aliyetoka katika kikosi cha Kadogoo.
Jambo la kushangaza leo, Mwana wa marehemu, Joseph Kabila anaonekana akiunganisha nguvu tena na Paul Kagame na Waasi wa M23 wanaoungwa Mkono na Rwanda, Kupanga mikakati ya kivita ili wafanikishe kumdondosha Rais Félix Tshisekedi.
Swali la watu wengi ni hili: Je Kabila amesahau Damu ya baba yake..??
Jibu ni hapana. Amesahau hisia, kaweka mbele maslahi binafsi.
1. Baba yake aliuwawa vipi na kwa nini Serikali ya Rwanda imekuwa ikitajwa sana..??
Laurent Kabila hakuwa Rais wa kawaida katika nchi ya Congo. Aliingia madarakani kwa msaada wa mataifa ya Rwanda na Uganda. Lakini alipofika Ikulu, alikataa kuwa kibaraka wa nchi hizo mbili. Alimkataa Kagame na Museveni wazi wazi na akawafukuza wanajeshi wao Julai 1998.
Rwanda ilijibu kwa vita. Ikaunda RCD, ikajaribu kumpindua kwa ndege ya kutua Kinshasa Agosti 1998. Laurent Kabila alinusurika kwa msaada wa serikali za Zimbabwe, Angola na Namibia.
Kuanzia hapo nchi nzima ya Congo ilijaa hofu, njama na majasusi. Januari 2001, Mlinzi wake Rashidi Kasereka alimpiga risasi. Serikali ilisema ni Mapinduzi yaliyoshindwa.
Lakini watu wengi Congo bado wanaamini mkono wa Kigali ulikuwepo kwa sababu ndiye aliyekuwa na sababu na uwezo wa kufanya hivyo wakati huo.
Hiyo ndiyo kumbukumbu yenye uchungu.
2. Kwa nini Joseph Kabila leo yuko upande wa serikali ya Rwanda..??
Hapa nakutajia sababu kuu tatu na zote ni za kisiasa, sio za kifamilia.
Kwanza, Adui yake namba moja sio Kagame ni Tshisekedi. Tshisekedi amemvua kinga ya Useneta, Amemfungulia kesi ya Uhaini, Amemtaifisha mali, na Amemuita hadharani Msaliti anaefadhili M23. Kabila anataka kurudi Ikulu au kumuondoa Tshisekedi. Hilo haliwezekani bila amshirika mwenye Jeshi, Pesa na Diplomasia na huyo ni Rwanda.
Pili, Tangu Mwaka 2024, Kabila amekimbilia katika Maeneo ya Mashariki Mwa-congo (Goma na Kivu) na Maeneo yote hayo yapo chini ya utawala wa M23/AFC ya Corneille Nangaa na M23 kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa inapata Silaha, Mafunzo na Amri kutoka Rwanda. Huwezi kukaa Goma, Kufanya Mikutano na kupanga vita dhidi ya Kinshasa bila kuruhusiwa na Kigali. Kukutana na Kagame ni lazima.
Tatu, Familia nzima ya Kabila bado inafanya Biashara kubwa kubwa katika Migodi ya Dhahabu na Coltan na Marafiki wengi wa familia hiyo ni Maafisa wa kijeshi wa huko Kivu na Rwanda. Huo mitandao haikufa na Vita vya 1998. Leo inafanya kazi tena kumpa nguvu Kabila.
3. Historia inajirudia.
Huu ndiyo ujinga wa viongozi wa Congo:
Laurent Kabila aliwekwa Madarakani na Rwanda 1997, Kisha akaja kugombana nao 1998 na akauawa 2001.
Baada ya tukio la kifo cha Laurent Kabila, Joseph Kabila akasaidiwa kikamilifu na Rwanda kuchukua Madaraka ya Baba yake, Uzuri akakaa nao vizuri kwa miaka 18, Hadi alipondoka Madarakani 2019.
Leo tena ameamua tena kuomba Msaada wa Rwanda Ili afanikishe mapango wake wa kumpindua kiongozi (Rais) aliyemrithi.
Kwa lugha rahisi sana: Joseph Kabila hana tatizo na Serikali ya Rwanda iliyomuua baba yake, Bali ana tatizo na Tshisekedi anayetaka kumuua kisiasa.