MBOKA NA BISO
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 794
- 793
Moja ya taarifa za awali, ni kwamba baada ya serikali ya USA kuingilia mgogoro wa kisiasa kati ya DRC na Rwanda, ni kwamba Marekani inaitaka kuhakikisha madini yake yote yanapelekwa tu Rwanda, ambapo kuna viwanda vya kusafisha madini yapatikanayo ukanda huu, wa maziwa makuu; na badae hayo madini kuuziwa kwanza Marekani; na ikiwa mahitaji ya Marekani yamefikia kiwango kinachohitajika, yaliyosalia yanaweza kuuziwa nchi nyingine.
Ikumbukwe kuwa bado China na Russia na wao pia wana mikono yao huko, na makubaliano haya hayawahusu, ila cha kujiuliza, je serikali ya Marekani itakubali kula sahani moja na wabaya wake, huku DRC ndo ina mamlaka ya mwisho kuhusu mali zake!? Je, itavunja mikataba na wachimbaji wengine!?
Rwanda imepataje dili hilo!? Kilichoifanya ijenge viwanda vyenye hadhi ya kimataifa huku ikiwa na kiasi kidogo cha madini ni nini!? Ilijuaje siku moja dili lingetiki!!!