VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,494
- 1,466
Inasemekana mpaka sasa, baada ya ndege moja kutoka Ulaya na inahisiwa kuwa ilileta silaha, uwanja wa ndege wa Bujumbura nchini Burundi, umekumbwa na hitilafu ya mfumo wa uongozaji wa ndege, jambo lililosababisha kusitisha kutua na kuruka kwa ndege katika uwanja huo. Jiji la Bujumbura, halina mtandao mpaka sasa.
Jeshi la Burundi, limeanza kuondoa wengi wa wanajeshi wake kurudi maeneo ya mpakani.
Juzi, Burundi ilimuondoa mkurugenzi wa shirika la Enabel, nchi iliyotoa mfumo huo wa uwanja wa ndege.
Jambo hilo linaendelea huku hali ya hofu ikitanda mjini Uvira, baada ya kundi la Wazalendo kumkataa mkuu wa kanda ya jeshi, Gen Gasita,alieteuliwa na raisi. Mpaka sasa, risasi kati ya wazalendo wanaomtuhumu kuwa mnyarwanda na mtumishi wa siri wa M23, na jeshi la FARDC linalotakiwa kuheshimu amri ya amiri jeshi mkuu kumuweka kiongozi aliemteua.