Ni ngumu kuzuia mauaji ya kifamilia

Ni ngumu kuzuia mauaji ya kifamilia

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,565
Reaction score
5,983
Polisi nchini Rwanda, imejibu malalamiko ya wananchi wa Rwanda, waliohoji inasaidia nini jamii, wimbi la mauaji linaloongezeka kwa kasi kati ya wanandoa.

Kwa kujibu,Polisi imesema si rahisi,kwa sababu mauaji hufanyika baada ya wanaoishi pamoja kuingia ndani mwao.

Mauaji yalishika kasi baada ya serikali ya Rwanda kuanzisha mfumo wa haki sawa.
Mfumo huu ulivuka majukumu ya kifamilia, ukawa wa maisha ya kawaida.
Nchini Rwanda, unyanyasaji wa kijinsia,kwa wanaume ni mwingi sana.Lakini ikitokea mwanamke akatoa malalamiko, basi mwanaume lazima apate hifadhi kwanza jela kwa muda.

Pamoja na mengine mengi yanayoendelea, hali hii ilisababisha wanaume wasioweza kuzuia hasira zao kuchukua maamzi ya kuwapiga na kuwaua wenza wao. Imefikia hatua wanandoa wanaua wake zao na watoto kwa pamoja, wakati mwingine kupoteza ushahidi wa chanzo.

Cha ajabu, wapo pia wanaume wanaouliwa na wake zao, kwa kupigwa shoka au jembe kichwani.
 
Back
Top Bottom