Mkuu wa majeshi wa Uganda, awataka raia wa Uturuki waishio nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo

Mkuu wa majeshi wa Uganda, awataka raia wa Uturuki waishio nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo

Tiziano

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
114
Reaction score
9
Mkuu wa majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amewataka raia wa Uturuki wanaoishi nchini humo kuondoka, huku akitangaza Maandamano makubwa mbele ya Ubalozi wa Uturuki mjini Kampala, Septemba 18.
Muhoozi, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, alisema kupitia mtandao wa X kwamba amekata uhusiano na maslahi ya Uturuki nchini Uganda na kuwataka raia wa Uturuki wafungashe mizigo yao na kuondoka.
Pia amemtaka Mbunge Twala Fadhil kuongoza maandamano hayo, huku akionya kuwa mtu yeyote atakayehusishwa na kuwa wakala wa Uturuki wakati wa maandamano anaweza kukamatwa.
Mvutano huo unahusishwa kwa kiasi kikubwa na Fred Lumbuye, mkosoaji wa serikali ya Uganda na mwanablogu anayeishi Uturuki.
Muhoozi amekuwa akiitaka serikali ya Uturuki kumrejesha Lumbuye nchini Uganda au kumfukuza.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna tangazo rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda linalothibitisha kwamba serikali imeweka amri rasmi ya kuwafukuza raia wote wa Uturuki.
Hatua hiyo inaweza kuongeza mvutano katika uhusiano kati ya Uganda na Uturuki, ambao unahusisha biashara, uwekezaji, miundombinu na elimu.
 
Back
Top Bottom