Maoni ya mdau kuhusu kichapo cha wa Houthi kwa Saudi Arabia

Maoni ya mdau kuhusu kichapo cha wa Houthi kwa Saudi Arabia

MBOKA NA BISO

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
794
Reaction score
793
Saudi Arabia inakila sababu ya kupigwa isitumie Maka na Madina kama ngao ya utawala wa kifalme:

Saudi Arabia si mshirika wa kawaida tu wa Marekani huko Mashariki ya Kati kama mnavyo Rahisisha.

Ndani ya Saudi Arabia kuna Prince Sultan Air Base nadhani kituo hicho mnakifahau.

Ni kituo cha kijeshi cha Saudia ambacho Marekani imekuwa ikikitumia kama sehemu muhimu ya uwepo wake wa kijeshi katika eneo hilo.

Tukirejea kumbukumbu za mwaka 2019 Marekani ilirejesha kwa nguvu uwepo wake katika kituo hicho ambacho kwa ufupi huitwa PSAB, na kituo hicho kikawa moja ya vituo muhimu vya U.S. Central Command (CENTCOM) kwa kuendesha na kuunga mkono nguvu za anga za Marekani huko mashariki ya kati.

Na hapa ndipo historia inakuwa nzito zaidi na yenye kuumiza japo wakereketwa wa Saudi Arabia wataona kama nina chuki na nchi hiyo ya kifalme.

Katika miaka ya nyuma, Prince Sultan Air Base ilikuwa kitovu kikubwa cha operesheni za anga za Marekani katika eneo hilo.

Wakati wa Operation Desert Storm dhidi ya Iraq mwaka 1991, Marekani iliendesha kampeni kubwa ya anga kutoka katika ukanda huo, U.S. Air Forces Central inaeleza kuwa ndege zake zilifanya zaidi ya Mashambulizi👉 29,000 na kudondosha zaidi ya tani 👉 60,000 za mabomu na silaha wakati wa kampeni hiyo.

Unahisi tani zote hizo zilikuwa zinauwa kitu gani huko Iraq?

Baada ya vita, uwepo wa Marekani Saudi Arabia uliendelea kupitia Operation Southern Watch, iliyohusisha utekelezaji wa eneo la kutoruhusu ndege za Iraq kuruka kusini mwa Iraq.

Na mwaka 2003, Prince Sultan Air Base ilikuwa bado ikitumika katika shughuli za anga zilizohusishwa na Operation Iraqi Freedom.

Wakati huo kulikuwa na takribani ndege 200 za muungano katika kilele cha vita.

Hata operesheni ya Afghanistan ilihusisha kituo hiki kwa kiwango cha juu cha uongozi wa kijeshi, Yani Kituo hicho kilitumika kuwaua Wataliban pamoja na familia za huko Afghanistan.

Kituo cha Combined Air Operations Center kilichokuwa Prince Sultan Air Base kilihusika katika kupanga kampeni ya anga ya Operation Enduring Freedom.

Kwa hiyo unapozungumzia uhusiano wa Marekani na Saudi Arabia, usiangalie tu mafuta, biashara na silaha.

Angalia pia jiografia ya kijeshi:

Saudi Arabia iko katikati ya eneo lenye migogoro mingi iloanzishwa na Marekani.

Iraq, Iran, Yemen, Bahari Nyekundu, Ghuba ya Uajemi na njia za kuelekea Afrika Mashariki.

Ndiyo maana Marekani yenyewe imeeleza kua Prince Sultan Air Base kama sehemu inayotoa operational depth kwa nguvu zake huko Mashariki ya Kati.

Kituo hicho kimewahi kuwa na F-15E, F-16, F-22, F-35 pamoja na ndege za upelelezi na udhibiti wa anga.

Kwa lugha rahisi naweza sema kwamba: ARDHI YA SAUDI ARABIA IMEKUWA SEHEMU MUHIMU YA MZUNGUKO WA NGUVU ZA KIJESHI ZA MAREKANI MASHARIKI YA KATI.

Na hapa ndipo tunapaswa kujiuliza swali moja kubwa:

Je, Saudi Arabia ni mshirika wa Marekani kwa sababu tu ya mafuta na biashara, au pia kwa sababu ardhi yake ina thamani kubwa sana kijeshi na kimkakati?

Hapo ndipo uchambuzi wa kweli wa uhusiano wa Washington na Riyadh unapoanzia.

Kwahiyo Saudi Arabia ijitafakari na iache kutumia Miji mitakatifu kwa Mujibu wa dini ya kiislamu kama Ngao.

Lazima Saudi Arabia na watu wake waonje machungu kama wengine wanavyoonja, vingenevyo inatakiwa kujitenga na migogoro mapemaaaaa. Na si vinginevyo, ni kuacha ukaribu na Marekani na kuondokana na kila kinachoihusu.
 
Back
Top Bottom