Willy NGOMA
JF-Expert Member
- Feb 25, 2016
- 4,565
- 5,983
Jamhuri ya Rwanda kupitia Wizara ya Elimu iliteuliwa kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya nne ya Siku ya Kiswahili Duniani. Kwa kuzingatia utaratibu wa kupokezana uenyeji kati ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), maadhimisho haya yatafanyika kuanzia tarehe 6 hadi 7 Julai 2025 katika Hoteli ya Serena, jijini Kigali.Tumsikilize Bi. Rose Baguma, Mkuu wa Idara ya Sera za Elimu katika Wizara ya Elimu ya Rwanda, akitoa ujumbe kuhusu tukio hili muhimu.