Kabila ameanza kumtikisa Rais Felix Tshisekedi .

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,567
Reaction score
5,983
Zikiwa zimepita siku chache tu tangu kutangazwa ķwa Joseph Kabila kuwa kiongozi wa kundi lililojiunga na waasi wa M23 la FRN tayari Raisi Felix Tshisekedi amaenza kuonja joto ya jiwe ambapo jana maafisa wa polisi nchini Belgium, wamavamia na kupekua nyumba za ndugu na washirika wa karibu wa Tshisekedi wanaoishi Belgium.
Sababu kubwa ni tuhuma ya utakatishaji fedha uliofanywa na Tshisekedi kwenye sekta ya madini nchini Congo.
Polisi pia wamepekua jumba la kifahari la Tshisekedi na mkewe lenye ukubwa wa square meter 860 kwenye eneo la square metre 7000 iliyopo jijini Brussels.

Hii ni baada ya kuibuliwa upya kwa ķesi ya madai ya utakatishaji fedha na ufisadi kwenye madini iliyofunguliwa mwaka 2025 na NGOs kadhaa nchini Congo.

Kaka wa Rais Tshisekedi bwana Tshisekedi Jacques, ameziita tuhuma hizo kuwa za uongo na zisizo na ushaidi kwa lengo la kumchafua mdogo wake.

Hii maana yake ni kuwa tayari Kabila ameanzisha chokochoko dhidi ya Tshisekedi.
 
Waafrica tuna shida sana, tunaiba mali za nchi zetu kwenda kuendeleza kwa wazungu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…