Dunia inazunguka kwa kasi, utajinyonga.Usipokuwa makini utajinyonga

Dunia inazunguka kwa kasi, utajinyonga.Usipokuwa makini utajinyonga

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,565
Reaction score
5,983
Wanaume wengi bado wanaishi kama watoto yatima....
Wanatoa kwa kila mtu lakini hakuna anayewapa wao kitu.
Wanalipa bills zote, kodi zote, wanakuwepo katika kila janga, wanalinda familia n.k.
Lakini wakichoka, hakuna anayewauliza mbona umepooza, mbona umekuwa mnyonge?
Sana sana utasikia huyu jamaa anajisikia sana siku hizi. Na wengine watasema siku hizi huyu jamaa kawa mdhaifu sana, lakini hakuna atakaye kujali au kukuuliza chochote.
Makuzi ya wanaume yamejengwa katika kuishi kiume, wengi hawajakuzwa katika kujua namna ya kuomba msaada na kuongea ukweli wamezidiwa. Wanaume wengi wanachagua kukaa kimya matokeo yake wanavunjika vunjika ndani yao kimya kimya na dunia inakuja kujua baadaye sana kuwa huyu kumbe alikuwa na shida, mara nyingi inakuwa too late.
Wanaume tuambiane ukweli sisi ni binadamu na tuna hisia, onyesha hisia zako. Hilo halitokufanya usionekane mwananaume. Na kuomba msaada wowote hata wa kimawazo, haitokufanya wewe uonekane ni mlaini (soft).
Hata kama wewe ni mwanaume mgumu, bado unahitaji kuyafurahia Maisha kivyako vyako, unahitaji kupata mapumziko, unahitaji kuhurumiwa na kutendewa wema. Coz wewe naye ni binadamu tu, usijifanye John Cena au Robot kisa uonekane kidume, speak out.
 
Back
Top Bottom