Watu wana ardhi zao toka enzi. Leo hii, walishazuiliwa kufanya chochote, baada ya kusema ni maeneo hatarishi, hivyo hayatakiwi kufanyiwa shughuli yoyote. Mpaka serikali iwalipe fidia, wakatafute sehemu zingine. Kabla ya jambo hilo, ndo hapo hapo wanapolima na kujitafutia chakula, kama kuomba tu ardhi.
Leo hii, wanatakiwa walipie ushuru wa kila mwaka wa ardhi. Kumbuka, ardhi ni mali ya serikali, hati miliki wanazopewa raia, ni kodi kwa muda wa miaka 99.
Hawa watu wasipolipa kodi, fidia hawapati.
Na je, kodi wanailipiaje serikali wakati iliwanyang'anya ardhi hiyo!