VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,494
- 1,466
Nchi ya Rwanda, kama nchi zote zinazojitafuta, jijini Kigali, usafiri wa haraka na wa uhakika ni pikipiki,maarufu kama bodaboda.
Kazi hii, inakisiwa kuwa na masirahi makubwa ukilinganisha na kazi nyingine nyingi.
Asilimia kubwa ya waendesha pikipiki, ni za mkataba.
Ni kazi iliyowezesha wengi kutunza familia zao,huko nyuma, mji wa mwendesha pikipiki, ulikuwa unasifika kwa maisha mazuri.
Ghafla, hali ikabadilika, leo hii ndo watu wenye maisha magumu kupita kiasi:
Chanzo kilitokana na Bima ya pikipiki kupanda,ambapo wengi husema ni zaidi hata ya pikipiki yenyewe.
Bima hulipwa kutokana na muda pikipiki iliotoka kiwandani. Kadri inavyokuwa na umri mkubwa, ndivyo gharama za bima zinakuwa kubwa pia.
Cha ajabu, haijalishi ni ya biashara au matumizi binafsi,gharama za bima ni zile zile.
Mbali na swala la bima, pia ni faini wanazotozwa na Polisi,kitengo cha usalama barabarani.
Rwanda ina mfumo wa kielectroniki. Ukiwa na chombo cha moto, kimesajiliwa hadi namba yako. Makosa mengi ni ya kamera za barabarani:
-Ukiwa mwenfo kasi, uwezekano wa kupata ujumbe ni mkubwa, maana 90% ya barabara za Rwanda, speed limit ni 60 KM/h.
-Wanaotumia barabara za mjini, kuna camera zilizopo kwenye makutano ya barabara. Huko kumechorwa mistari. Tairi ikikanyaga kwenye mstari, hilo ni kosa, na hapo hapo unaandikiwa faini.
-Kwa sasa, kuna drones zinazozunguuka mjini, na taarifa zinazotolewa na picha za drones hizo, mara nyingi huonesha umetenda kosa, na lazima uandikiwe faini.
- Kuna askali Polisi wengine, husimama kando ya barabara, hasa sehemu zenye msongamano, na kuandika plate number na makosa. Pia utastukia unatumiwa ujumbe.
Kosa lolote, unatakiwa ulipe ndani ya siku 3. Ukichelewa, inaongezeka elfu kumi (sawa na elfu 20 ya Tanzania).
Rwanda ina mfumo wa kuscan kila chombo cha moto kipitacho, kama una deni, huna pa kukimbilia. Ukishindwa kulipa kwa wakati, chombo chako kitapelekwa kituo cha polisi, na kikikaa miezi 3 bila kulipiwa, kinapigwa mnada.
Hapa ndo panakuja kilio cha boda boda: mara nyingi hudai kuonewa, na vyombo vyao kuchukuliwa. Gharama za bima, gharama za makosa wanayoandikiwa, gharama za maisha kwa ujumla, ni kubwa kuliko kipato chao.
Hii imesababisha wengi wao kufanya kazi kwa sababu hawana tu chanzo kingine cha kipato, ila raha ya kazi yao hawana tena.
Alipoulizwa mkuu wa Polisi, kitengo cha usalama barabarani, ACP Boniphace RUTIKANGA, alisema wanachotakiwa ni kutii na si vinginevyo,kwamba hakuna anaeonewa. Alisisitiza kwamba, kipindi wapo askali polisi kushughulikia hayo makosa, ilionekana wanawalalamikia kuwaonea, ndipo wakaanzisha mifumo ya kielektoniki, ambayo haimuonei mtu.
Kilio chao, baada ya kuona kwenye ngazi husika hakina jibu, wanasubiri mkuu wa nchi atoe tamko.