Trafiki bandia wakamatwa na waendesha bodaboda mjini Kigali

Trafiki bandia wakamatwa na waendesha bodaboda mjini Kigali

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,565
Reaction score
5,983

View: https://x.com/btntvrwanda/status/1917923701779018161

Pichani, ni badhi ya waendesha pikipiki jijini Kigali, nchini Rwanda, baada ya kumkamata mtu anaedai kuwa ni askali polisi, kitengo cha usalama barabarani.
Kama wanavyoeleza, mtu huyo amekuwa akiwapiga picha maeneo mbali mbali. Kawaida, wanaotakiwa kufanya hivyo, ni askari wenye mavazi ya kazi. Licha ya hivyo lakini, kumekuwepo na malalmiko ya mara kwa mara, ya waendesha pikipiki hao, kwa kupata messeji za makosa walioandikiwa na watu wasiowafahamu. Jambo hili lilihusishwa na utendaji kazi usiofaa wa Polisi, na kuituhumu kufanya uonevu wa hali ya juu kukusanya mapato.

Baada ya waendesha bodaboda hao kumshitukia mtu huyo, alikimbia na wao kuacha pikipiki zao na kumkimbiza. Ni baada ya kupiga picha plate number ya mmoja wao, alipogeuka, akamuomba amuonyeshe kadi ya kazi, na mtu huyu akaonekana kutokuwa na yo na kutaka kukimbia.

Nchini Rwanda, kumekuwa na wingi wa watu wanaotapeli watu kwa njia mbali mbali.

Mara kadhaa, watu wa namna hii, wamekuwa wakifuatwa na madereva bodaboda waliopigwa picha, ili wawafanie wepesi, kulingana na wingi wa faini, hivyo kuelewana na kupewa chochote ili wasiwalipoti makao makuu.
 
Back
Top Bottom