Tanzania: Waliopo darasa la tano, kumaliza shule ya musingi mwaka 2027

TX Noran

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
131
Reaction score
13
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na Wizara ya Elimu Tanzania wametia mabadiliko rasmi ya elimu ya msingi ambapo wanafunzi waliopo Darasa la Tano mwaka huu (2026) wanatarajiwa kumaliza elimu ya msingi mwaka ujao wa 2027 wakiwa Darasa la Sita.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Septemba 18, 202- iliyotolewa na NECTA, mabadiliko hayo yanatokana na utekelezaji wa Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 (Toleo la 2023), ambayo imepunguza muda wa elimu ya msingi kutoka miaka saba hadi miaka sita yaani kuanzia Darasa la 1 hadi la 6.

NECTA imeitaja 2027 kama mwaka wa Mpito ambapo wanafunzi hawatasoma Darasa la Saba, badala yake, watafanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) wakiwa Darasa la Sita mnamo mwaka 2027 na kisha kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2028.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…