Sababu(Badhi) za mwanaume kusalitiwa na mwanamke

Sababu(Badhi) za mwanaume kusalitiwa na mwanamke

Chegge

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
195
Reaction score
7
Wanawake Watakusaliti Ikiwa:

1. Wewe ni mwema kupita kiasi. Baba huruma, nice man.

2. Wewe ni mwanaume mwenye mapenzi kupita kiasi (Loverboy).
Unamweka mwanamke wako mbele ya kila kitu, kiasi cha kuamini falsafa isemayo, “Mke mwenye furaha, maisha yenye furaha.” 🚮
Wanawake wana tabia ya kuchukulia mambo mazuri wanayotendewa kuwa ya kawaida na kutoyathamini. Na wewe si kwamba utakuwa salama dhidi ya tabia hiyo.

3. Wewe ni mwanaume mwenye kung'ang'ania mwanamke kupita kiasi (Clingy).
Acha uking'ang'a.
Hakutaki muache. Usimtafute. Usibembeleze mbuzi yeyote. Hakuna kitu kinachoweza kumchukiza mwanamke zaidi ya mwanaume anayemtegemea kihisia kupita kiasi na kushindwa kumpa nafasi yake.
Hali hiyo huonyesha ukosefu wa heshima binafsi, kujithamini na hadhi ya kiume.

4. Unapatikana kila wakati (Always Available).
Wanawake wanahitaji nafasi na muda wa kukukumbuka, kukumisi na hata kuwaza kuhusu wewe wanapokuwa mbali nawe. Hivyo ndivyo ilivyo.
Ikiwa hafikirii kuhusu wewe wala hana hamu ya kukukumbuka mnapokuwa mbali, basi sahau kabisa habari hiyo.

5. Unasamehe kwa urahisi kupita kiasi (Easily Forgiving).
Hili ni kosa la mwanzo linalofanywa na wanaume dhaifu. Wanasamehe kirahisi kwa sababu wamefundishwa hivyo kanisani.
Lakini unapaswa kuelewa jambo moja: unapomsamehe mwanamke kirahisi bila kumfanya awajibike kwa makosa yake na kukabiliana na matokeo ya matendo yake, anaweza kuacha kukuheshimu.
Ataanza kuamini kwamba mipaka yako haina maana yoyote na kwamba huichukulii kwa uzito.
Matokeo yake, atarudia kosa hilo tena.

6. Kupenda wanawake wakuokoteza wasio wa viwango.



Source: Robert Heriel Tz
 
Back
Top Bottom