Baada ya Rwanda Investigation Bureau kuwasaidia watu wapatao 10, kurudi nchini wakitokea Myanmar,walikopelekwa na matapeli kwa ahadi ya kazi, uongozi wa RIB umefanya kikao na vyombo vya habari,kuviomba vifikishe taarifa kwa umma, kuwataka vijana wawe makini.
Kwa muda wa miezi 8 tu, wamerudishwa nchini watu 105, walikokuwa wakiteseka huko ugaibuni. Wengi wao hudanganywa kazi za mapokezi na wanaishia kufanya za ndani. Kipindi cha nyuma, mmoja alitoa ushuhuda wa alivyokuwa akilazimishwa na Boss wake mwarabu,kufanya mapenzi na mbwa wake.