Ntahakikisha, Rwanda itakuwa mkoa wa 26 wa DRC. Waziri Mutamba

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,494
Reaction score
1,466
Constant MUTAMBA(Pichani), alikuwa ameahidi kwamba atafanya kila analoliweza kuhakikisha Rwanda inakuwa mkoa wa 26 wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Badae, kupitia wizara yake ya sheria, aliwahukumu vijana wa mikoa mbali mbali waliotuhumiwa wizi,kwa lengo la kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la vijana hao waliokuwa na tabia ya kuwapora na kuwaibia mali zao. Vijana hao walipewa adhabu ya kifo, na walinyongwa.

Muda mfupi tu, badae, amepatikana na hatia ya kuiba Dola za Kimarekani Milioni 19, ambazo zilikuwa za kujenga gereza kubwa nchini humo. Kamati ya Senate ilimuvua wadhifa wake, ili mahakama iweze kumhoji.

Mpaka sasa, haruhusiwi kutoka nje ya jiji la Kinshasa. Na yupo chini ya uangalizi maalum.

Mtamba, ana umri wa miaka 37. Mihela yote hiyo kwa umri huo, isingemuacha salama




 
Hizo ni zilizojulikana,huenda kuna kwingine alishamega vitu. Sema tu kwa umri wake, ndo maana alikuwa na kibuli cha ajabu.
Na tunategemea Africa ijikwamue na iondokane na umasikini 🀣🀣🀣🀣

Wakati kuna mjinga kalalia 398Billion Tanzania shillings πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Africa, tulilogwa

Na katika jamii hiyo hiyo kuna mama au familia inawaza inalalaje bila kula ikiwa ni siku ya pili

Mungu naamini upo, na naamini utatenda siku moja hata kama si Leo basi siku yeyote kwa waja wako
 
Ndo maana tunastahili kutawaliwa tu. Wazungu hawana namna. Na nchi zote ni hayo hayo. Nyingine mbunge eti kasema, ombeni mikopo tu sisi tutapitisha msijali. Hahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…