Kwa wanaume tuuu. Watoto wa kiume,kaeni pembeni.

Kwa wanaume tuuu. Watoto wa kiume,kaeni pembeni.

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,565
Reaction score
5,983
MWANAUME kamwe usiombe ukakosa pesa au kazi au ukayumba kiuchumi kipindi ambacho ulijawa jeuri na kiburi kwa mke wako kisa mali alizo kukuta nazo au mlizo chuma pamoja.

Rafiki yangu kumbuka utakapo ishiwa jiandae kuteseka vya kutosha haswa kama ulitumia hizo pesa zako kuhonga wanawake wa nje na kulewa bar jiandae kuishi humo ndani kwa mateso mazito mpaka utatamani kuhama nyumba au nchi (si kila Mwanaume aliye achana na mke wake mwanamke ndiyo mkorofi, kuna wengine wanajiharibia wenyewe na kuamua kukimbia), Maana mrs yeye tayari anakuwa ameshazoea maisha yake ya msoto na kuhangaika na watoto na kujiwekeza kwenye vibiashara vyake, Hivyo kamwe hutokaa uitie machoni mwako pesa yake pengine huruma ya Mungu iingilie kati.

Hivyo basi mwanaume ukijipata huko kazini kwako kwa kupandishwa cheo au kupanda kiuchumi kamwe usimsahau mwanamke uliyo anza nae maisha au kuchuma nae hizo mali, si kila mwanamke ana hiyo nyota ya ushindi wengine nyota zao ni kama za mamba ukimuoa tu jiandae kuangamia baada ya kufanikiwa, ndiyo maana utasikia hii kauli "JAMAA TOKA KAOA MAMBO YAKE YAMENYOOKA SANA AU JAMAA TOKA KAOA AMEPOTEA KABISA"

Ukipata mwanamke wa kukuvusha kutoka Mahala fulani kwenda mahala pengine mshukuru sana MUNGU na mshikilie sana huyo Mwanamke cheza na vyote lakini usimharibie furaha yake.
 
Back
Top Bottom