Hii ni kauli ya msemaji mkuu wa jiji la Kigali, nchini Rwanda. Akiongea na vyombo vya habari, alitangaza kuwa, ukuaji wa jiji hilo, unaendana na uongezeko la wakazi kumiliki magari kwa ajiri ya safari zao binafsi.
Msemaji huyo, amesema kwamba hakuna sababu ya mtu kutumia usafiri wake ikiwa hana safari ndefu,kwa sababu maegesho jijini humo ni changamoto.
Siku za nyuma, Kigali ilitangaza nia ya kuhakikisha siku za usoni, watu wanaoingia mjini, wanatumia magari ya umma, huku parkingi zikiwekwa nje ya mji:
Maswali ya kujiuliza:
-1. Ikiwa mmiliki wa gari, alonunua kwa pesa yake, mafuta yake, ushuru na michango kibao, hatakiwi kutumia gari lake, lina faida gani?!
2. Uongozi unaposema utajenga maegesho nje ya mji, kwa hiyo, wamiliki wa magari jijini, watakuwa wanapeleka kwanza magari huko? Au ndo kusema hawataruhusiwa kuyatumia tena! Je, kutakuwa sasa na mfumo wa kuomba kibali kutumia gari mtu alonunu kwa hela yake?
3. Kila kukicha, raia wanalalamikia maamzi ya viongozi, yanayoleta suruhu kwa muda usipungua miaka miwili. Je, wanaohusika na mipango miji, wasomi, wana kazi gani!?
4.