Boda boda na akili zao kama za kina naniiii

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,494
Reaction score
1,466
KAMA ULIKUWA HUJUI VIZURI MAAJABU YA BODABODA WACHA NIKUFAHAMISHE:

1) Bodaboda ndio usafili ambao muda wote dereva anataka kuwahi, Ukimuuliza unataka kuwahi wapi hata yeye hapajui,

2) Bodaboda ndio usafili ambao unashindana na chochote kilicho mbele yake, Chochote kilicho mbele ya Bodaboda iwe gari au baskeli au Toyo, Bodaboda atakimbizana nacho Ili akipite,

3) Akili za Bodaboda wote ni kama zina fanana, Brother hata ukimuona Mkubwa kiasi Gani ilimradi tu ni Bodaboda, Basi wote akili zao ziko sawa sijui mafuta yana walevya au nini sijui,

4) Usije ukamwambia Bodaboda niwahishe haraka nimechelewa, Brother hilo ni kosa kubwa Sana utakua umefanya Kwa upande wako, lakini ni furaha kubwa sana Kwa bodaboda, Utajuta kuzaliwa na pengine kuanzia siku hiyo hutopanda tena bodaboda; Hii kauli wanapenda sana watu wa bodaboda, yaani ukimwambia hivyo anajisikia furaha kama vile ameokota mabilioni, atakukimbiza mpaka macho yatatoka machozi.

5) Bodaboda hawapendi kauli ya kuambiwa punguza mwendo, ukitaka kumkera bodaboda mwambie apunguze mwendo, hii kauli wanaichukia kupita maelezo,

5) Kuamini wao ndio wenye haki na barabara kuliko wenzao; bodaboda wao ndio hujiona wenye haki zaidi na barabara kuliko wenzao, ndio maana unaweza kukuta magari yamesimama Lakini wao wanapita tu, hasa sehemu za kuvuka kwa miguu usipokua makini wakati unavuka, Unaweza kugongwa na bodaboda hapohapo licha ya magari kusimama,

6) Hawapendi kitu kinachoitwa foleni barabarani, wakikuta foleni watajazana mbele kabisa ya magari ili foleni ikitembea wao wawe wa kwanza kupita, wakati mwengine watatafuta njia mbadala hata sehemu hatarishi, ila wao hawajali ilimradi wapite tu.

7) Ukipanda bodaboda wewe abiria ndie unatakiwa kuchunga usalama wako; usalama wako sio jukumu la bodaboda kuuchunga, ukimtegemea bodaboda umeliwa kwa sababu hata usalama wake yeye mwenyewe anakutegemea wewe abiria wake au chombo alichogongana nacho, Hata kama kosa ni lake yeye anajiona hana kosa kabisa.



BODABODA HAO JAMANI.




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…