VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,494
- 1,466
Wanawake jamani! Sijui laana! Maana hata Shetani wanaemsingizia, nina uhakika atakuwa anawacheka tu mkitaja jina lake.
Kamama hapo pichani, tayari kanaenda kutumikia kifungo cha maisha.
Alikuwa akifanya kazi za usafi majumbani kwa watu, ndipo siku moja alipoenda kibaruani kwa watu, akaamua amtupe mtoto wake chooni. Alimtupia kwenye choo chenye kina cha mita 20.
Kwa maelezo yake, alimshika mikono na kumning'iniza, akaingiza miguu kwenye tundu la choo. Baada ya kuona haingii, ndipo akaamua amshindilie kichwa, na mtoto kudumbukia.
Anadai chanzo ni kutelekezwa na mwanaume aliemzalisha. Jitihada za kumuokoa hazikuzaa matunda, maana mtoto alikutwa ameshafariki.
Wanawake, jitafakalini. Miaka miwili ni mingi, hata usipomtaka,kuna watu wapo tayari kulea, kuna wengine wanaweza kusaidia.
Watoto wa kiume wanaowaza tu kukojoa pasipo kukabili matokeo ya tamaa zao, hata nyie yakitokea kama haya, nafsi zinawasuta na kufanikiwa hamuwezi kamwe. Hizi laana haziwezi kuwaacha salama