Ni mwanamitindo maarufu nchini Rwanda, mmiliki wa Moshions Fashions Design, aliejizolea umaarufu kwa kuwashonea viongozi wakubwa na viongozi wa mataifa mbali mbali.
Hapo nyumba, kwenye ukurasa wake,aliandika maneno yaliyoleta utata, baada ya kuandika kuwa anamchukia Kagame na Inkotanyi wote. Alisema chanzo cha kuwachukia, akiwa na umri wa miaka sita (6), alimtembelea baba yake alipokuwa gerezani, na hakuruhusiwa hata kumsalimia, baada ya mlinzi kumpiga viboko(baba yake) na kumrudisha ndani.
Alipokamatwa, kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kutumia nadawa ya kulevya na kuyasambaza, inaposemekana alikutwa na bangi,kwa matumizi yake, na kwa kuwa alizitoa nchini Kenya, otomatikali ni muuzaji na msambazaji wa madawa hayo.
Kwa shelia ya nchi ya Rwanda inayohusu matumizi ya madawa ya kulevya, ukikutwa na hatia uuzaji na usambazaji, hupelekea kifungo cha maisha jera na faini ya faranga za Rwanda milioni 20(karibia 25 million Tshs).
Alikuwa bado anatumikia kifunga cha miaka mitatu, nje kwa dhamana, kwa kosa hilo hilo.
Huenda safari yake ya kufurahi maisha uraiani ikaishia hapa.