Baada ya ripoti kutoka ngazi za chini hadi ngazi za wilaya nchini Rwanda, kuonyesha kila kitu kipo sawa, kwa sasa vyombo vya habari vinaendelea kufichua mengi. Pichani, ni watoto wa chekechea, wasio na darasa, husomea chini ya mti. Walimu wao, wamesema ni changamoto kubwa, kwa sababu iwe jua au mvua ni wao na watoto hao, na kwamba huingia darasani tu muda wa chakula, baada ya kuazimwa na shule ya msingi iliyopo karibu.
Uongozi wa chini mara nyingi umekuwa ukihusishwa na matukio hayo, ambapo ripoti zilizopo wizalani huonyesha kila kitu kiko sawa, na mwisho wa siku raia wanazidi kulalamikia maumivu wanayopata, na kwamba uongozi wa ngazi za chini hauwasaidii,badala yake unawatuuhumu kuongopea vyombo vya habari.
View: https://www.youtube.com/watch?v=nROqfUkRLjw