Hari abavuga ko bafungirwa muri Tongati i Karongi
bakuwe mu mihanda nyuma y'amazi atanu bakabura uburyo bwo kugera aho batuye bikabasaba kugenda amanywa n'ijoro bagasaba ko bazajya bahabwa ubufasha mu gihe barekuwe.
Badhi ya raia, akiwemo na mwandishi wa habari, wamelalamikia vyombo vya habari kuhusu uonevu wanaofanyiwa na uongozi wa wilaya ya Karongi, Magharibi mwa nchi ya Rwanda.
Walipoulizwa, baada ya kukutana na vyombo vya habari, walielezea manyanyaso wanayopitia,huku wakiwa raia wasio na hatia.
Basi waliopelekwa kwenye vituo vya kuhifadhia waharifu, wamesema chanzo mara nyingi huwa ni zoezi la kuzoazoa watu, wengine wakiwa hawajatembea na vitambulisho vyao.
Wanasema wakanopelekwa huko, Tongati, hupelekwa na gari la wilaya. Lakini wanapoachiwa baada ya miezi mitano hadi 6(5-6), hujikuta wanalazimika kutembea kwa mguu umbali mrefu.
Wengine hulazimika kutembea usiku na mchana; na wanapokutana na dolia usiku, tena bila vitambulisho na maelezo ya kujitosheleza, hujikuta tena sehemu zingine au pale pale walikopelekwa mwanzoni.
Kwa kuwa uongozi hautaki kuwa waungwana, basi wameomba angalau wawe wanasaidiwa kurudishwa walikotolewa, kuweza kufika makwao kirahisi. Ni jambo ambalo uongozi wa wilaya umetupilia mbali, ukidai kwamba hizo gharama za mafuta kuwarudisha walikotoka, ni bora zikasaidie katika maeneo mengine yenye uhitaji.
Rwanda ina vituo karibu kila wilaya, vijulikanavyo kama Transit Centers.
Vituo hivi, vilifunguliwa kupokea waharifu na watumiaji wa madawa ya kulevya. Cha ajabu, mtu yeyote mwenye sauti, ukitofautiana nae, unaweza jikuta unabebwa.
Kwa waliowahi kukaa humo, wanasema maisha ni magumu na mateso ni makali kiasi cha kutamani bora wangekuwa wanapelekwa gerezani na kuhukumiwa. Watu hukaa kati ya miezi 6 hadi miaka miwili, kama huna wa kufatilia, huweza kukaa muda mrefu.