Wakimbizi hawa walikuwa wakiishi kambini Kakuma, huko Turkana, nchini Kenya.
Walioweza kutoa taarifa, wamesema uamzi huo ulitokana na kupunguzwa zaidi ya 50% ya chakula kutoka shirika la msaada kwa wakimbizi(UNHCR), na kuamua kurudi kwao, huku wakieleza kwamba hawana imani na usalama wao,nchini kwao.
Mmoja alisema kwamba, kilichofanya akimbie nchi yake, bado kipo pale pale, na kwamba kambini huko angekuwa na uhakika wa chakula, asingerudi.
Wakimbizi wengi kutoka Burundi, kwa sasa wanahifadhiwa na mataifa ya jirani na nchi hiyo, baada ya vurugu zilizotokana na jaribio la kupindua serikali ya aliyekuwa raisi mwaka 2015, hayati Pierre Nkurunziza.
Burundi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu siku za hivi karibuni.
Nchi nzima, hofu inazidi kutanda, kutokana na ghasia za hapa na pale, kutoka kwa vijana wanaopewa mafunzo ya kujihami, kutoka chama tawala cha CNDD-FDD.
Burundi inakabiliwa pia na kumimywa kwa uhuru wa vyombo vya habari, na kutopewa nafasi kwa vyama pinzani, ambapo wafuasi wengi wwamekuwa wakitiwa mbaloni na vyombo vya dola, wengine wakipoteza maisha, na wengine kutojulikana walipo.