Rwanda kuanza kuzalisha Gas ya kupikia majumbani

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,494
Reaction score
1,466


Pichani, ni mtambo wa kuvuta na kuchakata Gas iliyopo ziwani(Kivu), kati ya DRC na Rwanda. Gas hiyo ijulikanayo kama Methane, inajulikana kuwa ni hatari sana ikilipuka. Ziwa Kivu, lipo karibu na milima ambayo bado inatoa uji kutoka ardhini, ambao joto lake likikutana na gas hii, basi ni maafa na ingeweza kuua mamia ya watu na kuharibu viumbe hai vyote virivyo karibu na ziwa hili kwa muda mfupi. Baada ya utafiti kugundua kuwa wingi wake ni tishio, na kuna badhi ya nchi tayari maafa yalishatokea, kutokana na uwepo wake ziwani, serikali ya Rwanda, ililazimika kutafuta wataalamu na baada ya kubaini uwepo wake, zilianza jitihada za kuichimba.

Awali, watu walidhani gas hiyo, ingesaidia kupunguza gharama za gesi ya kupikia majumbani, lakini ilipoanza kuzalishwa, haikuwa ya kupikia, bali ya matumizi mengine.

Jitihada ziliendelea, na mpaka sasa, wataalamu walishapata njia za kuongeza matumizi yake ili iweze kutumika kwa ajili ya kupikia.

Mradi huu, mpaka sasa, unatoa gesi ambayo iligeuzwa kuwa umeme, na kuingiza kwenye gridi ya taifa la rwanda, umeme wa MW56.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…