Rais wa Kenya,atoa neno dhidi ya maandamano yanayoendelea.

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,494
Reaction score
1,466
Rais William Ruto ameagiza polisi nchini Kenya kutumia nguvu zaidi dhidi ya watu wanaojihusisha na uporaji au uharibifu wa mali wakati wa maandamano, akisema kuwa wanaopatikana wakifanya vitendo hivyo wapigwe risasi kwenye miguu ili kudhibiti machafuko

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa nyumba za bei nafuu eneo la Kilimani, Nairobi, Ruto ameelezea masikitiko yake kuhusu kile alichokitaja kuwa ni hali ya kipekee ya vurugu na upinzani mkali dhidi ya serikali yake.

Alitilia shaka kwa nini viongozi wa upinzani wamekuwa wakionesha msimamo mkali dhidi yake tofauti na walivyofanya kwa marais waliomtangulia kama Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta.

Kwa mujibu wa Ruto, haieleweki ni kwa nini fujo na maandamano yanalengwa kwake binafsi, huku akisema kuwa si haki kuendeleza siasa za chuki, kiburi na ukabila.

Alisisitiza kuwa Wakenya wote ni sawa na hakuna aliye bora kuliko mwingine, akitoa wito wa mshikamano wa kitaifa.


Habari kutoka East Africa radio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…