Bomoa Bomoa yaziacha familia nyingi nje nje

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,494
Reaction score
1,466



Serikali ifikie hatua iwahurumie raia wake.

Pichani, ni watoto wanne wa mama mmoja aliekuwa akilea mwenyewe. Baada ya zoezi la kamati ya jiji la bomoa bomoa kuanza, lilimuathiri. mama huyu, inasemekana alivunjia nyuma, hii ikiwa ni mara ya tatu. Alipowaona tu wanakuja kuvunja, alitoweka na kutokomea kusikojulikana, huku akiacha watoto 4, wa mwisho akiwa wa miezi nane(8). Waliovunja nyumba walimaliza na kuondoka, uongozi wa ngazi za chini ukaondoka, watoto hawakuwa na pa kwenda, ndo wakaamua walale humo humo kwenye nyumba yao iliyovunjwa.

Mpaka sasa, msaada wa ulinzi ni wa wananchi majirani tu,na wanachosema ni kwamba njaa imewafika pabaya watoto.

Nyumba hizi zisemekanazo kama zilizojengwa katika maeneo hatalishi, zinafikiwa na kila aina ya miundombinu, ikiwemo maji na umeme.

Wanaojiita wabunge, wapo tu mjini huko wanakula kodi za hawa walala hoi na machozi yao, hawaneni lolote, kama vile hawajui.
Wananchi wakati mwingine wana kila sababu ya kuuchukia uongozi na kukimbia nchi zao,kwa sababu ya uonevu.
Ni kweli wapo wanaojenga kinyemera, lakini hakuna nyumba inayojengwa usiku, na haiwezekani nyumba isimame,ipauliwe na watu wahamie,bila uongozi kujua. Sasa basi, viongozi wasiowajibishwa, ndo chanzo cha haya yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…